Dhana Kumi Kubwa kuhusu Uislamu (sehemu ya 1 kati ya 2): Ufikiaji wa Taarifa hauzuii dhana mbaya kuhusu uislamu
Maelezo: Kuangalia kwa kifupi dhana tatu kuu za mwanzo kuhusu Uislamu.
- Na Aisha Stacey (© 2014 IslamReligion.com)
- Iliyochapishwa mnamo 04 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 5,382 (wastani wa kila siku: 5)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Tangu Waislamu walipo fagiliwa nje ya Rasi ya Kiarabu ili kuunda Dola ya Kiislamu kumekuwa na dhana na vumi zinazo zunguka kuhusu njia ya Waislamu wanazoishi. Karibia miaka 1500 iliyopita ibada ya kumuabudia Mungu Mmoja zimebadilisha dunia tunayoijua, ila dhana bado zinauzunguka Uislamu japokuwa watu wa dunia wana kiwango kikubwa cha taarifa. Ndani ya sehemu hizi mbili za makala tutaangalia dhana 10 ambazo dunia zinasababisha kutokuelewana na kuvumiliana.
1.Uislamu unahimiza ugaidi.
Katika miongo miwili ya Karne ya 21hii inaweza kuwa dhana kubwa kuhusu Uislamu. Kipindi ambacho dunia inaonekana kuwa na kichaa kwa kuuwa watu wasio na hatia ikumbukwe kuwa dini ya uislamu iliweka sheria maalumu ya vita na kuweka thamani kubwa ya maisha.
"...aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote...." (Kurani 5:32)
Mauaji ya watu wasio na hatia imekatazwa. Kipindi Mtume Muhammad, rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake, alipotuma maswahaba wake kwenye mapigano alisema "Nendeni kwa jina la Mungu na msiuwe mzee, mtoto mchanga, kijana, au mwanamke. Sambaza wema na tenda wema, kwasababu Mungu anawapenda wanaofanya wema."[1] "Msiwaue watawa kwenye nyumba zao za ibada" au "Na msiwaue watu waliokaa sehemu zao za ibada.[2] Wakati mtume alipoona maiti ya mwanamke ardhini na akasema, "hakuwa anapigana. Imekuwaje akauwawa?"
Kanuni hizi ziliendelea kufuatwa na Caliph wa kwanza wa Dola ya Kiislamu, Abu Bakr. Alisema, "Ninawaamuru vitu kumi. Msiuwe wanawake, watoto, au wazee, mtu dhaifu. Msikate miti ya matunda. usiharibu sehemu ya makazi. Usiuwe kondoo au ngamia labda tu kwa chakula. Usiwaunguze nyuki au kuwatawanya. Usiibe kutoka kwa mateka, na usiwe muoga."[3] na cha kuogezea katika haya Waislamu wamekatazwa kufanya vitu visivyofaa. Haijaruhusiwa kuuwa mtu ambaye ajakufanyia uadui.
"Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanao kupigeni, wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi waanzao uadui…" (Kurani 2:190)
2.Uislamu unawanyanyasa wanawake.
Uislamu unawaheshimu wanawake haijalishi wapo katika hatua gani ya maisha yao. Akiwa mtoto, anafungua milango ya pepo ya baba yake.[4] Akiwa mke, anakamilisha nusu ya dini ya mumewe.[5] Akiwa mama, Pepo iko chini ya miguu yake.[6] Wanaume wa kiislamu wanatakiwa kuwaheshimu wanawake katika kila hali kwasababu Uislamu unataka mwanamke aheshimiwe na apewe usawa.
Kwenye Uislamu mwanamke, kama mwanaume, wamelazimishwa kumuamini Mungu na kumuabudia Yeye. Wanamke yupo sawa na mwanaume katika swala la malipo ya baadae.
"Na anaye fanya mema, akiwa mwanamume au mwanamke, naye ni Muumini - basi hao wataingia Peponi wala hawatadhulumiwa hata kadiri ya tundu ya kokwa ya tende." (Kurani 4:124)
Uislamu umempa mwanamke haki ya kuwa na mali na kuthibiti pesa zake. Inampa mwanamke haki kamili ya kurithi na haki ya elimu. Mwanamke wa Kiislamu ana haki ya kukubali au kukataa ombi la ndoa na yupo huru katika matakwa ya kuhudumia na kuendeleza familia hivyo mwanamke anayefanya kazi yupo huru kuhudumia mahitaji ya nyumbani, au kutohudumia, akiona inafaa. Uislamu imempa mwanamke haki ya kuomba talaka kama ni lazima.
Inahusunisha ni kweli wanawake wengine wa Kiislamu wanaonewa. Kwa bahati mbaya wengi hawajui haki zao na kuwa wahanga wa ukiukwaji wa kitamaduni ambao hauna nafasi kwenye Uislamu. Watu wenye nguvu, vikundi na serikali kudai kuwa Waislamu ila wanashindwa vibaya kutekeleza kanuni za Uislamu. Kama wanawake wakipewa haki zao walizopewa na Mungu, kama zilivyowekwa kwenye dini ya Uislamu, Ukandamizaji wa wanawake ungesagwa na kusahaulika. Mtume Muhammad amesema, "Hakuna mwingine bali mwanaume mwenye heshima tu ndiye anayemtendea mwanamke kwa heshima . Na hakuna mwingine bali asiyejielewa tu ndiye hamuheshimu mwanamke."[7]
3.Waislamu wote ni Waarabu
Dini ya Uislamu imefunuliwa kwa watu wote, katika sehemu zote, muda wote. Uislamu ulifunuliwa kwa lugha ya Kiarabu na Mtume Muhammad alikuwa Muarabu, ila itakuwa siyo sahihi kufikiria kuwa Waislamu ni Waarabu, au kwa maana hiyo, Waarabu wote ni Waislamu. Hata hivyo Waislamu wengi wapo bilioni 1.57 [8] Ambao siyo asili ya Waarabu.
Japokuwa watu wengi, sana sana wa magharibi, wanauhusisha Uislamu na nchi za Mashariki ya Kati, kulingana na Kituo cha Uchunguzi cha Pew takriban theluthi mbili (62%) ya Waislamu wanaishi ukanda wa Asia Pasifiki na kiuhakika waislamu wengi wanaishi India na Pakistani (milioni 344 ukizichanganya) zaidi ya Mashariki ya Kati na Ukanda wa Afrika ya Kaskazini (milioni 317).
Pia kutokana na Pew, "Waislamu wanafanya idadi kubwa katika nchi 49 ulimwenguni. Nchi yenye idadi kubwa (takribani milioni 209 ) ni Indonesia, ambayo 87.2% ya idadi ya watu wanachukuliwa kuwa Waislamu. India ni ya pili kidunia kuwa na idadi kubwa ya Waislamu (kwa wastani milioni 176) Japokuwa Waislamu wanafanya 14.4% ya idadi yote ya watu wa India."
Uislamu sio asili au kabila - ni dini. Hivyo Waislamu wanaweza na kuwa katika sehemu yoyote ya dunia kuanzia alpine tundra ya Scandinavia hadi maji ya moto ya pwani ya Fiji.
"Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane..." (Kurani 49:13)
Vielezi-chini:
[1] Abu Dawood
[2] Imam Ahmad
[3] Tabari, Al (1993), Ushindi wa Uarabuni, Chuo kikuu cha New York Press, uk. 16
[4] Saheeh Muslim. ndani ya Ahmad na Ibn Majah msichana mtoto anajulikana kama "kingio la moto" kwa baba yake.
[5] Al-Bayhaqi
[6] Ahmad, An-Nasai
[7] At-Tirmidhi
[8] Kutokana na nakala, "Utambuzi wa Idadi ya Waislamu Ulimwenguni," na jukwaa la Pew kwenye Dini & Maisha.
Ongeza maoni