Mtu wa mwisho kuingia Peponi (sehemu 1 kati ya sehemu 2): Na Mti Utatokea.

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Atakapo tambaa mtu wa mwisho nje ya Jahannamu, na atakapoingizwa Peponi, milango ya Jahannamu itafungwa milele.

  • Na Aisha Stacey (© 2013 IslamReligion.com)
  • Iliyochapishwa mnamo 11 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 10 Sep 2023
  • Ilichapishwa: 1
  • Imetazamwa: 6,534
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

LastPersonEnterParadise1.jpg Pepo ni thawabu ya ajabu ambayo Mwenyezi Mungu amewaandalia Waumini, kwa wanao mt'ii Yeye. Ni mahali pa furaha kamili na utulivu na hakuna kitu ulimwenguni ambacho kinaweza kuvuruga utulivu huu. Itaendelea milele na tunatarajia kuwa itakuwa nyumba yetu ya milele. Kile ambacho Mungu na Mtume wake Muhammad wametuambia kuhusu Paradiso kinaweza vurumisha vichwa vyetu na akili zetu. Katika hadithi moja ya Mtume Muhammad, Mungu anasema: "Mimi nimewaandalia waja wangu wema ambao jicho halijapata kuuona, wala sikio halijapata kuusikia wala haujawahi kufikiriwa na akili za mwanadamu yeyote."[1] Hii ndio sisi, wanadamu, tumekuwa tukisubiri, na tukiwa na hekima na tuifanyie kazi, basi hii ndiyo malipo ya mapambano ya maisha haya ya muda mfupi. Tunatafakari na kujiuliza maswali kuhusu makao yetu ya milele, tunafikiri kuhusu Pepo kwa kuitamani na Jahannamu kwa kuihofia, lakini hata kama nyoyo zetu hutetemeka, mawazo ya Paradiso huleta furaha.

Maelezo ya peponi na Jahannamu katika hadeeth za Mtume Muhammad zina masimulizi kuhusu nani atakuwa mtu wa kwanza kuingia Peponi. Siku Kuu ya Kiyama Mtume Muhammad ndiye atakuwa mtu huyo. Aliwaambia wenzake kuwa atakuwa “wa kwanza kubisha kwenye milango ya Peponi”.[2]Na Mtume Muhammad alisema: "Nitakuja kwenye milango ya Pepo na nitaomba ifunguliwe. Mlinzi wa mlango atauliza, “Wewe ni nani?” Nitasema: 'Muhammad' Mlinzi wa mlango atasema “Niliamrishwa nisifungue mlango kwa mtu mwingine yeyote kabla yako”.[3]

Mtume Muhammad anaingia kwanza, na hiyo ni heshima anayoustahili. Itakuwa rahisi kwa Akili zetu kuelewa sababu za heshima hii kubwa, lakini baada ya muda fulani tunaanza kujiuliza ni nani atakayekuwa mtu wa mwisho kuingia Peponi. Kwa sababu kutakuwa na mtu wa mwisho na kisha milango itafungwa. Masahaba wa Mtume Muhammad pia walishangaa kuhusu Paradiso kwa namna ile ile tunayofanya sisi. Hata hivyo walikuwa na fursa ya kipekee ya kuweza kumuuliza Mtume wao mpendwa ni nani hasa atakayekuwa mtu wa mwisho kuingia Peponi?

Kama tunavyojua mapokeo ya Mtume Muhammad yanakuja kwetu kwa namna mbalimbali na mojawapo ya hayo ni hadith qudsi au hadith takatifu. Hadithi hizi ni muhimu hasa kwa sababu huku maneno yanasemwa na Mtume Muhammad, maana yake hutoka kwa Mwenyezi Mungu. Ni aina ya ufunuo. Hadithi hizi zinaunda mwelekeo mwingine wa ujumbe wa Mungu kwa wanadamu na kwa kawaida hushughulikia masuala ya kiroho au ya kimaadili. Jibu la swali lililoulizwa na masahaba linapatikana katika hadith qudsi na ni mojawapo ya hadeeth nzuri sana. Yafuatayo ni tafsiri ya hadeeth hii.

Mtu wa mwisho kuingia peponi atakuwa mtu ambaye atatembea kiasi, kisha akajikwaa mara na kuchomwa na moto mara nyingine. Mara atakapokwisha kuupita, atageuka na kukabiliana nao akisema: 'Ahimidiwe Yule Aliyeniokoa na wewe. Mwenyezi Mungu amenipa kitu ambacho hakumpa wa kwanza wala wa mwisho.'

Kisha mti utainuliwa mbele yake, naye atasema: 'Mola wangu Mlezi! Nipeleke karibu na mti huu, ili nipate kukaa chini ya kivuli chake na kunywa maji yake,' na Mwenyezi Mungu Mwenye Utukufu wote, atasema: 'Ewe mwana wa Adam nikikupa hili, utaniomba kitu kingine?' Atasema: 'Hapana Mola Mlezi!' Naye ataahidi kuwa hatamwomba chochote kingine, na Mola wake Mlezi atamsamehe kwa sababu ameona kitu ambacho hawezi kujizuia nacho. Basi ataletwa karibu nayo, naye atakaa katika kivuli chake na kunywa maji yake.

Kisha ataonyeshwa mti mzuri zaidi kuliko ule wa kwanza, na atasema: 'Mola wangu Mlezi! Nipeleke karibu na mti huo, ili nipate kunywa maji yake na nikae chini kivuli chake, wala sitakuomba kitu kingine chochote,' na atasema: 'Ewe mwana wa Adam hukuniahidi kuwa hutaniuliza kitu kingine chochote?” Atasema: 'Nikikuleta karibu nao huenda ukaniomba kitu kingine,' naye ataahidi kuwa hutamwomba chochote kingine, na Mola wake Mlezi atamsamehe kwa sababu ameona kitu ambacho hana kujizuia nacho. Basi ataletwa karibu nao, naye atakaa katika kivuli chake na kunywa maji yake.

Kisha atainuliwa mti mwingine kwenye mlango wa Pepo, ambao ni mzuri zaidi kuliko wa kwanza, na atasema: 'Mola wangu Mlezi! Nipeleke karibu na mti huo, ili nipate kukaa chini ya kivuli chake, na niyanywe maji yake, wala sitakuomba chochote kingine.' Atasema: 'Ewe mwana wa Adam! Kwani hukuniahidi kuwa hutaniomba chochote kingine?' Naye atasema: 'Naam, Ewe Mola, sitakuomba chochote kingine.' Mola wake Mlezi atamsamehe kwa sababu ameona kitu ambacho hana subra ya kujizuia nacho. Ataukaribia, na atakapo kuja karibu atasikia sauti za watu wa Peponi, na atasema: 'Mola Mlezi! Niingize humo.' Atasema: 'Ewe mwana wa Adam! Ni nini kitakacho kuacha kuuliza tena? Je, itakuridhisha nikikupa ulimwengu na mfano wake tena?” Atasema: 'Ewe Mola Mlezi! Unanidhihaki na hali Wewe ni Mola Mlezi wa walimwengu wote?'

Ibn Mas'ood (sahaba anayesimulia simulizi hii nzuri) alitabasamu na kusema: Kwa nini hamniulizi kwanini nina tabasamu? Wakasema: Kwa nini unatabasamu? Akasema: Hivi ndivyo Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alitabasamu, na wao ( masahaba waliokuwa karibu naye) wakamuuliza: Kwa nini unatabasamu, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Kwa sababu Mola Mlezi wa walimwengu wote atatabasamu anapo sema: Je! Unanidhihaki na hali Wewe ni Mola Mlezi wa walimwengu wote? Na (Mwenyezi Mungu) atasema: Mimi sikukudhihaki, lakini mimi ni Muweza wa kutenda nitakavyo.’”[4]

Katika sehemu ya pili tutajadili jinsi fadhili na rehema za Mungu zinavyoonyeshwa katika hadithi hii na kuangalia jinsi Mola wa walimwengu wote anavyojua vizuri na kuelewa uumbaji wake.



Vielezi-chini:

[1] Saheeh Al-Bukhari, Saheeh Muslim

[2] Saheeh Muslim

[3] Ibid

[4] Saheeh Muslim

Mbaya Nzuri zaidi

Sehemu za Makala hiki

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi
(Soma zaidi...)

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.